Habari
SHILOLE AHUISHA TAARIFA ZA JINA LA BIASHARA YAKE
Mwanamuziki na Mfanyabiashara Bi. Zena Yusuph almaarufu "Shilole" amehuisha taarifa za Jina la Biashara yake #Shishi Food katika Mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS), leo tarehe 31 Machi, 2023 Kijitonyama Mabatini, jijini Dar es Salaam.
Baada ya kukamilisha mchakato huo, Shilole amewataka wafanyabiashara wengine wanaotumia majina ya biashara bila ya kuyasajili Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), kuyasajili ili kuyalinda kisheria na kuepuka watu wengine kujinufaisha nayo.
Pia ameipongeza BRELA kufanya kazi kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kuwafikia wadau popote walipo na kuwapatia huduma.