Utangulizi
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ilianzishwa chini ya Sheria ya Wakala za Serikali Na. 30 ya Mwaka 1997 na kuzinduliwa rasmi tarehe 3 Desemba 1999 chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara. Majukumu ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ni kama yalivyoainishwa kwenye Waraka wa Uanzishwaji (establishment order) Na. 38 ya Tangazo la Serikali na. 294 la tarehe 08/10/1999.