Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni

Tunaipa Uhai wa Kisheria Biashara yako

Habari

Tanzania yashiriki Mkutano wa Kidiplomasia wa Ukamilishwaji wa Mkataba wa WIPO wa Sheria ya Maumbo Bunifu


 

Tanzania yashiriki Mkutano wa Kidiplomasia wa Ukamilishwaji wa Mkataba wa WIPO wa Sheria ya Maumbo Bunifu

Mheshimiwa Balozi Dkt John Simbachawene, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Kidiplomasia wa Ukamilishwaji na upitishaji wa Mkataba wa Sheria ya Maumbo Bunifu wa Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (Diplomatic Conference on the Finalization and Adoption of the World Intellectual Property (WIPO) Design Law Treaty) akimuwakilisha Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo, mkutano huo umefanyika kuanzia tarehe 11 hadi 22 Novemba, 2024 huko Riyadh, Falme za Saudi Arabia.

Mkataba wa WIPO wa Sheria ya Maumbo Bunifu unalenga kuweka mfumo rahisi na wezeshi wa ulinzi wa Maumbo na Michoro Bunifu katika ngazi ya Kimataifa kwa wabunifu kutoka nchi Wanachama wa WIPO zitakazoridhia Mkataba huo.

Mkutano huo wa Kidiplomasia ulikamilishwa tarehe 22 Novemba, 2024 ambapo Nchi 17 Wanachama wa WIPO walipitisha Mkataba wa Riyadh wa Sheria ya Maumbo Bunifu (Riyadh Design Law Treaty).

Kwa upande wa Tanzania walioshiriki pia ni Mhe. Dkt. Moh’d Juma Abdallah, Balozi wa Tanzania katika Falme za Saudi Arabia, Bw. Godfrey Nyaisa, Afisa Mtendaji Mkuu kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bi. Loy Mhando Mkurugenzi wa Miliki Ubunifu kutoka BRELA, Bw. Mustafa Haji, Mrajisi Msaidizi kutoka Wakala wa Biashara na Mali Zanzibar, na Bw. Henry Bakaru, Mkurugenzi wa Sheria kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara.