Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni

Tunaipa Uhai wa Kisheria Biashara yako

Habari

ELIMU YA BRELA YAWAFIKIA VIZIWI KONDOA


ELIMU YA BRELA YAWAFIKIA VIZIWI KONDOA

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni BRELA umetoa elimu kuhusu huduma za Taasisi kwa watu wenye ulemavu wa kusikia (viziwi) katika wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma.

Elimu hiyo imetolewa Leo Februari 6, 2024 kwa lengo la kuhamasisha kundi hilo muhimu ili kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu huduma zinazotolewa na BRELA.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Afisa Leseni Kutoka BRELA Bi. Winfrida Gaudence amesema kuwa Taasisi imeitikia ombi la Taasisi ya Maendeleo kwa Viziwi Tanzania (TAMAVITA) la kuwapatia elimu hiyo ambayo ni yenye manufaa kwa biashara zao.

Ameeleza kuwa faida za kurasimisha Biashara BRELA ni pamoja na kuwa na upekee katika soko la huduma, kuwanufaisha pale wanapohitaji mikopo katika taasisi za kifedha, kuwafungulia fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na fursa za ukuzaji wa biashara.


" Niwapongeze kwa mwitikio wenu na nifuraha yetu kujumuika nanyi Ili kuwapatia elimu hii ya urasimishaji wa biashara na ninaamini mtakwenda kuitumia na vilevile kwa sababu tupo hapa basi kwa wale watakaohitaji msaada tupo kufanikisha hilo," ameongeza Bi. Gaudence

Sambamba na hilo amewaomba wenye vikundi vya kibiashara kusajili majina yao ya biashara au kampuni na kupata Leseni ili iwe rahisi kufanya biashara kwa uhuru zaidi.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TAMAVITA ameipongeza BRELA kwa kufika wilayani Kondoa na kukutana na watu wenye ulemavu wa kusikia na kuwapatia elimu ambayo itawasaidia kujikwamua na kusonga mbele zaidi kwenye biashara zao.

" Naomba kwanza niwaombe mumfikishie salamu Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA kuwa tunashukuru sana kwa kufadhili na kufanikisha mafunzo haya, niwahikikishie watu wenye ulemavu wa kusikia kuwa elimu waiyoipata leo itafungua fursa zaidi kwani wapo wafanyabiashara, wakulima na hata wajasiriamali ambao waliihitaji sana elimu hii," ameongeza Bw. Nyema

Mafunzo hayo ya siku moja yaliyofadhiliwa na BRELA yamewakutanisha viziwi zaidi ya 50 ambao kwa umoja wao wamesema wamehamasika na watakuwa maba