Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni

Tunaipa Uhai wa Kisheria Biashara yako

Habari

BRELA YATOA ELIMU KWA WAJASIRIAMALI TWCC, SABASABA


 

BRELA YATOA ELIMU KWA WAJASIRIAMALI TWCC, SABASABA.

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), leo Julai 06, 2024 imetoa elimu ya umuhimu wa kurasimisha biashara kwa wajasiriamali zaidi ya 200 wa Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), wanaoshiriki maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam, Sabasaba.


Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha wafanyabiashara hao kutambua faida za kufanya biashara iliyorasimishwa kisheria ikiwepo kupata urahisi wa masoko ya bidhaa zao ndani na nje ya nchi.


Naye, Rais wa Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Bi. Mercy Silla ameishukuru BRELA kwa kuendeleza mashirikiano na chemba hiyo kwa kufanya kazi pamoja na kuwafanya vijana na wanawake kutambua umuhimu wa kurasimisha Biashara.


"BRELA imekuwa taasisi inayofanya kazi kwa karibu na TWCC kwa kutoa elimu kwa wafanyabiashara, tumekuwa tukishirikiana kwenye makongamano mengi na wanawake wamekuwa wakirasimisha biashara zao kutokana na utaratibu mzuri walioweka" alisema Bi. Mercy Silla, Rais wa TWCC.


Kwa upande wake Afisa Wanachama kutoka Chemba ya Wanawake wafanyabiashara Tanzania (TWCC),Bi. Cresensia A. Mbunda amesema kati ya wanawake 200 waliopata mafunzo hayo ni wafanyabiashara 50 pekee bado hawajarasimisha biashara zao na wanaotarajia kurasimisha katika maonesho ya Sabasaba.


Nao, baadhi ya wanawake wajasiriamali waliopata mafunzo ya kurasimisha biashara kutoka BRELA akiwemo Eveline Kisanga na Wilbert Mbilinyi wameiomba Wakala kuendelea kutoa mafunzo mara kwa mara kwa wafanyabiashara ili waweze kunufaika na fursa za masoko zinazojotokea ndani na nje nchi.


BRELA bado inaendelea kutoa huduma zake zote katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam, Sabasaba. inapatikana karibu na banda la Wizara ya Fedha na pia katika jengo la Wizara ya Viwanda na Biashara