Habari
BRELA YAIGALAGAZA RAS MARA
BRELA YAIGALAGAZA RAS MARA
Timu ya mpira wa Pete ya wanawake ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), inayoshiriki katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI), imeibuka na ushindi baada ya kuigalagaza timu ya RAS Mara magoli 25 kwa matatu.
Timu hizo zimechuana leo tarehe 2 Oktoba, 2023 katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha (RUCU) mkoani Iringa.
Timu ya BRELA imeonesha ubabe wake ikiwa ni mchezo wa nne tangu kuanza kwa mashindano hayo Septemba 29, 2023.
Mashindano hayo yenye lengo la kuimarisha mahusiano mazuri kwa watumishi na kuimarisha afya zao yatahitimishwa rasmi tarehe 14 Oktoba, 2023 kwenye viwanja vya Samora mkoani humo.