Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni

Tunaipa Uhai wa Kisheria Biashara yako

Habari

BRELA YABEBA TUZO YA USHINDI WA TATU WA JUMLA YA BANDA BORA SABASABA


BRELA YABEBA TUZO YA USHINDI WA TATU WA JUMLA YA BANDA BORA SABASABA

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imebeba tuzo ya ushindi wa tatu wa jumla wa banda bora katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwa mwaka 2024.

Tuzo hiyo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Mhandisi Filipe Jacinto Nyusi ambaye alikua mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho hayo akiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

Akizungumza baada ya upokeaji wa tuzo Bw Godfrey Nyaisa Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA amesema ushindi huo umetokana na kujiwekea malengo ya ushiriki katika utoaji wa huduma bora kwa wafanyabiashara wanaorasimisha ndani ya uwanja wa maonesho na pia kutengeneza mazingira rafiki yenye kuwavutia ili kila anayepita aone umhimu wa kurasimisha biashara