Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni

Tunaipa Uhai wa Kisheria Biashara yako

Habari

BRELA YATOA USAIDIZI WA URASIMISHAJI BIASHARA


Na Mwandishi wetu:

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewahamasisha wafanyabiashara kutumia mfumo wa usajilikwa njia ya mtandao kurasimisha biashara zao kwa kusajili majina na alama za biashara.

Afisa Usajili Msaidizi wa BRELA Bi. Mary-Glory Mmary alitoahamasa hiyo wakati wa kampeni maalum ya kamilika naBRELA  2022 iliyofanyika katika viwanja vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Bi. Mmary alisema katika kipindi hicho cha kampeni maafisawa BRELA walitoa usaidizi kwa wafanyabiashara waliokuwa nachangamoto katika kufanya usajili mbalimbali kwa njia yamtandao.

“Changamoto kubwa iliyojitokeza ni baadhi ya wafanyabiasharakushindwa kutumia mfumo wa usajili kwa njia ya mtandaopamoja na jinsi ya kuwasilisha nyaraka mbalimbali hasa kwaupande wa makampuni na majina ya Biashara ,” alifafanua Bi. Mmary.

Aliongeza kuwa kampeni hii imeweiwezesha BRELA kutambuachangamoto wanazopitia wadau katika masuala ya matumizi yamfumo hivyo zoezi hili litaendelea katika mikoa yote yaTanzania.

Attachments area

Pichani Msajili msaidizi wa BRELA Bi. Mary-glory Mmary (kushoto) akikabdhi cheti kwa mmoja wa wadau waliokamilisha taratibu za usajili wa jina la biashara katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam.