Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni

Tunaipa Uhai wa Kisheria Biashara yako

Habari

BRELA YAWATAKA MAAFISA BIASHARA KUZINGATIA SHERIA


Na mwandishi wetu:

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewataka maafisa biashara kuzingatia sheria na kanuni wanapotoa leseni ya biashara kundi A na B ili kutoisababishia hasara serikali.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa biashara  wa mikoa ya Mwanza, Geita,  Simiyu, Mara na Kagera ili waweze kutekeleza majukumu kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa.
“Mathalani kwa mfanyabiashara anayesambaza bidhaa ya kinywaji nchi nzima anapaswa kuwa na leseni ya biashara kundi A, lakini kwa bidhaa zinazouzwa ndani ya mkoa ni leseni ya kundi B inayopaswa kutolewa kupitia halmashauri ya eneo husika,”alifafanua Bw.
Leseni ya Biashara kundi A hutolewa na BRELA kwani ndiyo yenye mamlaka wakati manispaa na halmashauri za miji zimepewa mamlaka ya kutoa leseni za Biashara kundi B. 
BRELA  inaendelea kuboresha mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao ili utoaji wa leseni kundi B pia ufanyike kwa njia ya kielektroniki kama ilivyo kwa leseni za biashara kundi A. 

 

Pichani Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Muhandisi Evalist Ndikilo (kushoto) wakizungumza jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Godfrey Nyaisa kabla ya kufungua mkutano wa maafisa biashara mkoani Mwanza.