Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni

Tunaipa Uhai wa Kisheria Biashara yako

Habari

BRELA YATOA ELIMU YA ULINZI WA BUNIFU VETA


BRELA YATOA ELIMU YA ULINZI WA BUNIFU VETA

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imetoa elimu kwa walimu na wanafunzi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA). Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo kuhusu haki miliki, usajili wa bunifu na namna ya kulinda vumbuzi dhidi ya wizi au matumizi yasiyo halali.

Akiwasilisha Mada Afisa Usajili kutoka BRELA Bw. Stanislaus Kigosi amesema kwamba kipindi hiki vijana wa VETA wamekuwa wakionesha uwezo mkubwa wa kubuni mashine, bidhaa na teknolojia mbalimbali. Amesisitiza kuwa bunifu yoyote iwe ni kifaa, huduma au hata chapa ya biashara ni mali ya mbunifu, na inapaswa kulindwa kisheria kwa kusajiliwa.

“Unapobuni, unaunda mali. Lakini usipoilinda, unaweza kuikosa.” amesema Kigosi

Ameeleza kuwa Kwa kulinda bunifu, wabunifu wanajihakikishia kuwa wao ndio wamiliki halali wa kile walichobuni, na wanaweza kupata faida ya kifedha kupitia leseni au kuuza haki miliki hizo, na pia wanapata heshima na kutambuliwa kama wabunifu halisi. Aidha, ulinzi wa bunifu huchochea ari ya kuendelea kuvumbua zaidi, kwa kuwa wanafunzi na walimu wanakuwa na uhakika kuwa kazi zao zitathaminiwa na kulindwa.

Kupitia Mafunzo mbalimbali BRELA imekua ikiwakumbusha na  kuwahimiza wadau wake kulinda Bunifu zao kwa kuzisajili ili ziwanufaishe na  kuwapa fursa mbalimbali katika Masoko.