Habari
MWALIKO WA KUWANIA TUZO ZA SHIRIKA LA MILIKI UBUNIFU DUNIANI KWA MAWAKA 2025 (2025 WIPO GLOBAL AWARDS)
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imepokea mwaliko kutoka Shirika la
Miliki Ubunifu Duniani (WIPO) kwaajili ya wafanyabiashara wa Tanzania kuwania Tuzo
za WIPO kwa Mwaka 2024. Muda wa kutuma maombi ni kuanzia Januari 15 hadi Machi
31, 2025.
Tuzo za WIPO zinatolewa kimataifa, na zinalenga kutambua na kusherehekea
mchango wa wajasiriamali wadogo na wakati, (SMEs) katika kutumia Miliki Ubunifu
katika uendeshaji wa biashara, na kuleta mabadiliko chanya kiuchumi, na kijamii kwa
ujumla.
BRELA inawahamasisha wajasiriamali wadogo na wa kati kuchangamkia fursa hii na
kushiriki katika kinyang’anyiro cha 2025 WIPO Global Awards katika sekta zote za
uchumi kama; nyanja ya kiteknolojia, kilimo, viwanda vya ubunifu au nyanja nyingine na
kutuma maombi ili kupata tuzo hizo.
Maombi yanaweza kutumwa kwa lugha ya Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Kirusi au
Kijapani. Jopo la waamuzi litachagua hadi washindi saba watakaoalikwa kuhudhuria
hafla ya Tuzo wakati wa Mkutano Mkuu wa WIPO utakaofanyika Julai, 2025 Geneva
Uswizi.
Jopo huru la majaji litachagua hadi washindi saba ambao wataalikwa kuhudhuria
sherehe za Tuzo wakati wa Mkutano Mkuu wa WIPO huko Geneva Uswizi.
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya Tuzo za WIPO Duniani
https://www.wipo.int/global-awards/en/how-to-apply.html na kwa usaidizi zaidi wasiliana
na BRELA kupitia simu namba +255 (0) 22 221 2800.
Imeandaliwa na;
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma